Tuesday, February 10, 2009

Ifanye siku ya Valentine iwe kumbukumbu kwenu


Siku ya Valentine ni siku ya furaha kwa wapendanao ambapo wengi huitumia kuoneshana mapenzi ya dhati walionayo kwa ampendaye lakini mbali na kufanya hivi siku hii ni vema wapendanao wakaitumia kupanga malengo ya maisha ya baadaye.Siku hii si siku ya kufuja pesa kwa wale walio na mapenzi ya dhati kwani hakuna haja ya kufanya maamuzi makubwa huku mkisahau kuwa kuna mambo mengi ya msingi mnayopaswa kufanya.

Mfano badala ya kutafuta zawadi kubwa na kwenda kupata chakula cha usiku kwenye hoteli ya kifahari mnaweza kutumia fedha hizo kununua vitu ya ndani kama siyo kuwalipia ada watoto wenu kama mnao.Unaweza kabisa kufurahia valentine na mwenza wako bila kwenda kula chakula cha usiku kwenye hoteli ya kifahari, kumnunulia zawadi, maua mwaka huu na kuwafanya muikumbuke siku hii daima. Bila shaka unajiuliza inawezekanaje? Zifuatazo ni dondoo zitakazokusaidia kusherehekea valentine yako kwa namna ya pekee:

1. Epuka kwenda kula chakula cha usiku hotelini.

Hoteli na migahawa mingi yenye hadhi duniani kote katika siku ya valentine huwa bize na zaidi gharama za vyakula hupanda hivyo ni vema ukamuandalia chakula akipendacho mpenzi wako nyumbani bila kujali kama wewe ni mwanaume au mwanamke kisha kumuandalia mezani huku mishumaa ya huba ikiangaza na mwanga hafifu.

2. Andika vitu 10 -15 ambavyo unavipenda kwa wa huba wako.

Andika sentensi fupi kila jambo unalolipenda kutoka kwa mwenzi wako kisha bandika kwenye kuta za sebule au chumbani kwako kisha tulia uone jinsi umpendaye atakavyofika nyumbani na kupigwa na butwaa akiangaza na kusoma vikaratasi ulivyobandika hakika atafarijika!

3. Sherekeheni chumbani kwenu.

Nunuani vinywaji mvipendavyo na crisps, pop cone au karanga zitakazowaburudisha katika picnic yenu mnayoifanyia chumbani badala ya ufukweni kama ilivyozoeleka na wengi lakini unapaswa kuhakikisha unawasha mishumaa kadhaa ili kupata mwanga hafifi na kama una taa ya rangi yenye mwanga hafifu unaweza ukaiwasha badala ya mishumaa kisha sherehekeeni kwa kujadiliana pamoja siku yenu na mipangilio ya maisha yenu ya baadaye.

4. Jipangieni malengoo.

Amini usiamini kwa kufanya hivi mtajikuta mmetawaliwa na hisia za huba kwani kila mmoja wenu ataweza kujifunza jambo jipya toka kwa mwenzake na kushirikishiana malengo mliyojiwekea ndani ya mwaka huu na kusaidiana mbinu za kuweza kutimiza malengo hayo pamoja na ndoto nyingine mlizonazo, lakini hakikisheni manaandika njia mbadara mlizojadili katika kutimiza ndoto zenu ili muweze kupitia mara kwa mara na kuwa na kumbukumbu na malengo mliyoyafikia na yale yaliyobadirika. Hii itawapa furaha na faraja kubwa siku za usoni kuona jinsi gani maisha yenu yamefanikiwa kwa kutumia vema siku ya valentine.

5. Elekeza mawazo yenu juu ya kudumisha upendo wenu huku mkitaniana.

Kila mtakachokubaliana hakikisheni mnawekeana sheria chake kwa usiku huo kama ‘hakuna kuwasha TV’. Hata kama mtatumia muda wenu chumbani mkicheza michezo ya kimahaba au kuzungumza mambo Fulani ya mapenzi, elekezeni hisia zenu za mapenzi kwa umpendaye yaani huyo uliyonaye chumbani na tanianeni ili mcheke pamoja.

Mfanyie mambo ambayo unahakika mpenzi waku hufurahia pindi unapomfanyia lakini fanya katika namna ya pekee ili ajione kuwa ni wa pekee kwako. Nakuhakikishaia hii itakuwa ni valentine ya pekee kwenu.Natambua wasomaji wangu wengi ni wasichana na wanawake na nimeaini kuwa, kitu pekee wanachokipenda ni wapenzi au waume zao kuwafanyia haya niliyoyaeleza. Kweli, lakini jaribu kumuonesha nwazi jinsi gani unampenda na kumthamini kwa usiku huo wa valentine.

Naamini atafurahia na ipo siku atajihisi kuwa na deni analotakiwa kukulipa kwa mahaba na mapenzi ya dhati uliyomuonesha nap engine itakuwa ni kukutunzia heshima yako kwa kutokuwa na mwanamke mwingine! Jaribu hili, naamini utafarijika kwa kufanikiwa kulifunfua kama si kuliimalisha penzi lenu.Hakika kwa kufanya hivi siku hii ya wapendanao kwenu itakuwa ni moja kati ya siku ambazo mtazikumbuka kwa muda mrefu na itaimalisha mizizi ya penzi lenu kama lililegalega. Kila la kheri katika kusherehekea siku hii ya valentine, Happy Valentine's Day!

2 comments:

Anonymous said...

endelea kutuelimisha wanajamii kwa ujumla kwani sio wote wanaoweza kuwa uelewa au kutambua jinsi haya mambo yanavyofanya kazi.

kaza buti mzee

Anonymous said...

nimefurahishwa sana na mada yako na Mungu akusaidia uzidi kutuelimisha.Nakutakia kazi njema na valentine njema.

Post a Comment

TOMA MAONI YAKO HAPA!