Thursday, September 10, 2009

NIMEAMBIWA NIFUNGE BLOG HII!

WADAU LEO NIMEKUMBANA NA EMAIL HII KWENYE BARUA PEPE YANGU, NIKAONA NISHEE NANYI WENZANGU KISHA KWAYOYOTE ATAKAYEJISIKIA KUTOA MAONI YAKE AWE HURU NAMI NIYABANDIKA HAPA, ILA MWISHO WA UJUMBE HUU TOKA KWA IBRA MOLLLEL NITAMJIBU KIMTINDO:-

Ndungu yangu messenger zako nimesisoma kupitia blg, lakini Je ungekua unatuma messenger kupitia NENO LA MUNGU, Mungu agekupenda sana na kufurai kwa sababu wewe unawapa watu wake habari njema, Mpendwa ktk Bwana nakushahuri umtafute yesu mapema kabla hajarudi. akakukuta katka mambo ya dunia. na mambo ya dunia hii yana pita lakini NENO LA BWANA halita pita kamwe, Soma yohana 3.16 utaona upendo wa Mungu Baba alivyo tupenda. uwemakini sana, damu ya Yesu isije ikawa ilimwagika buri kwako,

Acha kuwandikia watu mambo ya kimapenzi au kufundisha mapenzi badala ya KUFUNDISHA HABARI ZA UFALME WA MUNGU, BIBLIA INA SEMA KWA MANENO YAKO UTAHESABIWA HAKI NA KWA MANENO YAKO UTAHUKUMIWA,
sasa nimangapi uliyo ya fanya na kufundisha watu wa MUNGU mapenzi badala ya NENO LA MUNGU WAO, KUBALI WOKOVU WA MUNGU UPONE,

Ibrahim Mollel

Brazatk najibu:-
Asante kwa maoni yako bwana Ibra ila naomba uelewe kuwa katika dunia ya leo mamilioni ya watu walioko kwenye uhusiano wa mapenzi na ndoa wana ujuzi wa hali ya chini sana kwa kutojua mengi kuhusu viungo vya uzazi, matendo ya kimapenzi kwa sababu kuu moja, mambo ya jando na unyago hakuna tena! hivyo basi hivi sasa kila mtu hujifunza masuala ya mapenzi kwa kusoma sehemu mbalimbali!

Ibra naamini Mungu hachukizwi kwa mimi kutumia muda wangu kuwapa watu kitu wanapenda kwani shuleni niliposoma nilisoma saikologi of love, relationship na marriage na kama haitoshi mwalimu wangu Mr Nyamubi alinieleza kuwa "ili ujue elimu yako imekusaidia lazima ujuwe kuitumia kwa jamii inayokuzunguka!" akimaanisha kuwa lazima uisaidie jamii yako kwa elimu uliyoipata hivyo hichi ndicho nachokifanya hapa na katu sitakiacha kwani wengi nimewasaidia ndoa zao wanazifurahia na wengine mapenzi yao yaliyokuwa yamewachachia sasa ndoa zinanukia, HAKIka sitaacha kublog masuala ya mapenzi!

IBRA HUYU HAPA KWENYE PICHA KATIKATI NDIYE MR NYAMUBI ( ANAFANYA PHD UD HIVI SASA, MANENO YAKE NDIYO YALIZALISHA BLOG HII, KUSHOTO NI MMOJA KATI YA WANAFUNZI WALIOMALIZA TUMAINI TULLY (AFISA UTALII WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII) NA KULIA NI MIMI WAKATI WA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA ILIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM MWEZI WA SITA MWAKA HUU.
Ushauri wangu kwako ibra, kwakuwa teknologia ya blog ni rahisi kuitumia, naomba anzisha blog ya neno la Mungu nami nitakuwa msomaji wako namba moja na hata wasomaji wangu nitawashauri kupitia kwenye blog yako na nitaitangaza kwa nguvu zote ili neno lako liwafikie wanajamii!

NB: Katika miaka takribani 4 niliyojihusisha na shuguli hizi za kutoa ushauri wa mapenzi, uhusiano na ndoa kama ungekuwa ni mfuatiliaji mzuri wa mada mabalimbali nilizokuwa nazitoa magazetini (Ijumaa, Risasi, Amani na kwenye mtandao wa Global Publishers) utagundua kuwa ndani yake nimekuwa nikitumia maandiko ya dini hasa ya kiislamu na kikiristo hivyo nazani kwa nafasi yangu hapo inatosha.

NASHUKURU KWA USHAURI WAKO IBRA LAKINI NASIKITIKA SITAWEZA KUFANYA HIVYO, MUNGU AKUANGAZIE NURU YAKE NA KUKUPA UJASIRI WAKUTHUBUTU KUANZISHA BLOGU YA MAMBO YA DINI!

0 comments:

Post a Comment

TOMA MAONI YAKO HAPA!