Thursday, February 19, 2009

Marafiki/Wachumba

Mimi naitwa PETER MACHERA wa Mkoa wa Mara Musom (m)
Nina umri wa miaka 19.
Kazi yangu ni fundi wa Computer
Nahitaji Rafiki wa kike mwenye umri wa miaka 19 na
kuendelea.
Kwa mawasiliano zaidi simi No. 0713 131 676 au Email. P_machera@yahoo.co.uk

Hi everyone! Naitwa Gabriel from ARUSHA,natafuta marafiki wa kike,umri miaka 25 had 29,lengo ni urafiki wa muda mrefu had ndoa, sibagui kabila,rang awe mweupe or maji ya kunde,dini awe mkristo or mwislam ambae ataweza badilisha dini, tumia namba hii
255757518832, email255757518832@vodamms.co.tz

peogratius@yahoo.comBrazatk kupitia blog yako natafuta marafiki wa kike tu, wenye miaka 18--35. Sifa awe mwenye afya njema na mwenye uchungu na maisha.

Naitwa danny, umri wangu 24, elimu yangu chuo in short am banker natafuta mchumba ambaye atakakuwa mke wangu , napenda awe na umri kuanzia 18-24, elimu awe form four na kuendelea, pia awe mrefu mwembamba mwenye shepu ya mvuto na mweupe kiasi, dini awe mkristo na mwenye kumcha mungu, namba yangu ni 0714655049 na pia anitafute kwenye danful84@yahoo.com sms zitajibiwa on time.

Naitwa Lucy Massawe umri wangu 26, natafuta marafiki kokote ulimwenguni kuanzia miaka 28-35. Nchi ninayoishi Tanzania (Moshi) email mankatarimo@yahoo.com,
simu 0767 590944

Tuesday, February 10, 2009

Love Sms za VALENTINE!!!

1. …….. mtoto una jina tamu, linalonitia hamu yakuwa nawe mahali patamu patakapotufanya tusiishiwe hamu, yakuongea maneno matamu, sijui waweza nipa nafasi nikueleze yaliyo kwenye yangu nafsi siku ya valentine?

2. Mume mwenye hekima hasiti kuonesha hisia zake kwa mke wake na si kimada chake siku ya wapendanao, najua unanipenda na katu huwezi nitenda! Valentine imewadia sitegemei utanitenda, luv u mwaaah.

3. Naapa abadani penzi langu sitalitoa asilani ingawa upo mbali nami, nakupenda amini kwako nimefika, nitunzie langu penzi wasije niibia washenzi, valentine nyema mpenzi.

4. Mawingu yametanda napanda kwenye kitanda, macho nayaangaza, taratibu navuta shuka na kujitanda, mishumaa pembezoni inaniangaza, mziki laini wanibembeleza kitu pekee nilichokikosa ni joto lako na vijimambo vyako kunako kitanda! Valentine njema.


5. Nilikueleza lakini hukutaka kunisikia sasa wabaki ukilia-lia na leo wataka nirudia kwa maneno matamu kuniambia kisa valentine imewadia, najua hujatulia, siwezi moyo wangu kukufungulia, utabaki ukijutia lakini penzi siwezi kukupatia.

6. Natafuta maneno matamu ya kukukwambia mzazi wangu uliyenileta katika hii dunia, siku ya wapendanao ina/mewadia nami sina budi zawadi kukupatia hakika najivunia kwa malezi bora mliyonipatia. Happy Valentine mummy and dad

7. Siku zote nakaa nikijiuliza kwanini niliamua kuwa nawe maishani, kuishi mume na mke ni kazi lakini si kwako mpenzi unayejua kunienzi, mahaba matamu kunipatia, hakika siwezi jutia, nafsi yangu kukufungulia. Valentine njema mume wangu kipenzi.

8. Masomo yananitatiza, mapenzi yananitatiza, najiona kama nipo kwenye usiku wa giza, kwa jinsi ulivyoniumiza, wajua kiasi gani umenichukiza lakini mpenzi nakupenda basi punguza kunitenda. Be good, happy Valentine.

9. Nimefungua benki ya hisia za huba moyoni mwangu kwa ajili yako mpenzi, hivyo usisite kuhifadhi mahaba yako kujaza akaounti yako valentine hii kwani nitakupa riba nono ya huba. Nakupenda valentine njema.

10. Hisia za mapenzi hufikishwa kwa umpendaye kwa njia nyingi nami hsisa zangu kwako naziweka wazi kwa mtu anayesoma meseji hii, nakupenda itakupenda mpenzi. Valentine njema.

Ifanye siku ya Valentine iwe kumbukumbu kwenu


Siku ya Valentine ni siku ya furaha kwa wapendanao ambapo wengi huitumia kuoneshana mapenzi ya dhati walionayo kwa ampendaye lakini mbali na kufanya hivi siku hii ni vema wapendanao wakaitumia kupanga malengo ya maisha ya baadaye.Siku hii si siku ya kufuja pesa kwa wale walio na mapenzi ya dhati kwani hakuna haja ya kufanya maamuzi makubwa huku mkisahau kuwa kuna mambo mengi ya msingi mnayopaswa kufanya.

Mfano badala ya kutafuta zawadi kubwa na kwenda kupata chakula cha usiku kwenye hoteli ya kifahari mnaweza kutumia fedha hizo kununua vitu ya ndani kama siyo kuwalipia ada watoto wenu kama mnao.Unaweza kabisa kufurahia valentine na mwenza wako bila kwenda kula chakula cha usiku kwenye hoteli ya kifahari, kumnunulia zawadi, maua mwaka huu na kuwafanya muikumbuke siku hii daima. Bila shaka unajiuliza inawezekanaje? Zifuatazo ni dondoo zitakazokusaidia kusherehekea valentine yako kwa namna ya pekee:

1. Epuka kwenda kula chakula cha usiku hotelini.

Hoteli na migahawa mingi yenye hadhi duniani kote katika siku ya valentine huwa bize na zaidi gharama za vyakula hupanda hivyo ni vema ukamuandalia chakula akipendacho mpenzi wako nyumbani bila kujali kama wewe ni mwanaume au mwanamke kisha kumuandalia mezani huku mishumaa ya huba ikiangaza na mwanga hafifu.

2. Andika vitu 10 -15 ambavyo unavipenda kwa wa huba wako.

Andika sentensi fupi kila jambo unalolipenda kutoka kwa mwenzi wako kisha bandika kwenye kuta za sebule au chumbani kwako kisha tulia uone jinsi umpendaye atakavyofika nyumbani na kupigwa na butwaa akiangaza na kusoma vikaratasi ulivyobandika hakika atafarijika!

3. Sherekeheni chumbani kwenu.

Nunuani vinywaji mvipendavyo na crisps, pop cone au karanga zitakazowaburudisha katika picnic yenu mnayoifanyia chumbani badala ya ufukweni kama ilivyozoeleka na wengi lakini unapaswa kuhakikisha unawasha mishumaa kadhaa ili kupata mwanga hafifi na kama una taa ya rangi yenye mwanga hafifu unaweza ukaiwasha badala ya mishumaa kisha sherehekeeni kwa kujadiliana pamoja siku yenu na mipangilio ya maisha yenu ya baadaye.

4. Jipangieni malengoo.

Amini usiamini kwa kufanya hivi mtajikuta mmetawaliwa na hisia za huba kwani kila mmoja wenu ataweza kujifunza jambo jipya toka kwa mwenzake na kushirikishiana malengo mliyojiwekea ndani ya mwaka huu na kusaidiana mbinu za kuweza kutimiza malengo hayo pamoja na ndoto nyingine mlizonazo, lakini hakikisheni manaandika njia mbadara mlizojadili katika kutimiza ndoto zenu ili muweze kupitia mara kwa mara na kuwa na kumbukumbu na malengo mliyoyafikia na yale yaliyobadirika. Hii itawapa furaha na faraja kubwa siku za usoni kuona jinsi gani maisha yenu yamefanikiwa kwa kutumia vema siku ya valentine.

5. Elekeza mawazo yenu juu ya kudumisha upendo wenu huku mkitaniana.

Kila mtakachokubaliana hakikisheni mnawekeana sheria chake kwa usiku huo kama ‘hakuna kuwasha TV’. Hata kama mtatumia muda wenu chumbani mkicheza michezo ya kimahaba au kuzungumza mambo Fulani ya mapenzi, elekezeni hisia zenu za mapenzi kwa umpendaye yaani huyo uliyonaye chumbani na tanianeni ili mcheke pamoja.

Mfanyie mambo ambayo unahakika mpenzi waku hufurahia pindi unapomfanyia lakini fanya katika namna ya pekee ili ajione kuwa ni wa pekee kwako. Nakuhakikishaia hii itakuwa ni valentine ya pekee kwenu.Natambua wasomaji wangu wengi ni wasichana na wanawake na nimeaini kuwa, kitu pekee wanachokipenda ni wapenzi au waume zao kuwafanyia haya niliyoyaeleza. Kweli, lakini jaribu kumuonesha nwazi jinsi gani unampenda na kumthamini kwa usiku huo wa valentine.

Naamini atafurahia na ipo siku atajihisi kuwa na deni analotakiwa kukulipa kwa mahaba na mapenzi ya dhati uliyomuonesha nap engine itakuwa ni kukutunzia heshima yako kwa kutokuwa na mwanamke mwingine! Jaribu hili, naamini utafarijika kwa kufanikiwa kulifunfua kama si kuliimalisha penzi lenu.Hakika kwa kufanya hivi siku hii ya wapendanao kwenu itakuwa ni moja kati ya siku ambazo mtazikumbuka kwa muda mrefu na itaimalisha mizizi ya penzi lenu kama lililegalega. Kila la kheri katika kusherehekea siku hii ya valentine, Happy Valentine's Day!